
Timu ya Manchester United imefanikiwa kuingia kucheza michuano ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Nahodha Wayne Rooney aliifungia United bao la kwanza akimalizia pass kutoka kwa Anthony Martia na hilo likiwa bao lake la 100 kufunga Uwanja wa Old Trafford, Marcus Rashford akapachika goli la pili na baadaye Ashley Young kumalizia la tatu.